Mapigano katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo yanatajwa kuwa ni vita vyenye athari kubwa zaidi baada ya Vita Kuu ya Pili ya dunia.
Watu wapatao milioni tano wanakadiriwa kuuawa katika mapigano hayo katika moja ya nchi zenye utajiri mkubwa zaidi wa rasilimali duniani.
Idadi hii ya vifo (achilia mbali mateso) inahusisha makundi mengi wakiwemo wapiganaji, raia na hata waandishi wa habari, ambao wamekuwa wakilalamikia mazingira ya kazi nchini humo.
Abou Shatry wa Jamii Production amehojiana na mmoja wa waandishi wa Habari aliyeko nchini humo Al-Hadji Kudra Maliro ambaye ameeleza changamoto wanazokabiliana nazo katika kazi zao.
KARIBU UUNGANE NAO
No comments:
Post a Comment