Hivi punde tutasikia taarifa ya harakati za kuzuia uvutaji
sigara nchini Marekani ambazo sasa zimeamsha wasiwasi mwingine baada ya
kugundulika kuwa harakati hizohizo zimeifanya idadi ya wavutaji walio kati ya
darasa la 6-12 kuongezeka maradufu.
Lakini kwanza tuangalie habari za msiba ulioikumba jamii ya
waTanzania waishio maeneo ya Washington DC.
Marehemu Martha Shani
Uvutaji sigara, ni
sababu kubwa ya vifo vinavyozuilika nchini Marekani. Kwa mujibu wa
takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kudhibiti Maradhi nchini Marekani
(CDC) kifo kimoja kati ya vitano nchini Marekani hutokana na athari za
uvutaji sigara, na zaidi ya watu milioni 43.8 nchini humo ni wavutaji wa
sigara.
Lakini vita dhidi ya uvutaji huo vimekuwa vikipamba moto, na
teknolojia imekuwa ikishirikishwa katika vita hivyo. Na ni vita
hivyohivyo dhidi ya uvutaji vinavyoanza kutiliwa mashaka nchini humo.
Hii
ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA
DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 26, 2013
No comments:
Post a Comment