Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kulia) alipofanyiwa mahojiano na Mwanachangamoto yetu kutoka Jamii Production Mubelwa Bandio kuhusu oboreshaji wa huduma ya Tanzanite. Siku ya Jumatano Oct 9, ofisi ya Ubalozi Jijini Washington DC.
Dkt. Charles Kimei ameelezea kwamba, Mpango mzima wa akaunti ya mteja ikishafikisha kiwango fulani haitakuwa na makato ya kila mwezi na sasa CRDB umeanzisha huduma mpya kwa wana Diapora wa Tanzania inayojulikana kama Jijenge ambayo ni kutoa mikopo ya nyumba yenye lengo la kuiweka Diapora karibu na nyumbani.
Akitoa mfano mdogo Dkt. Charles kwa waTanzania wapendao kununua magari ya kifahari kabla hata kuwa najumba kuwa unaweza kuwa na gari lako lakini si salama siku gari likipata ajali utabaki huna kitu lakini nyumba itakufanya hata unaporudi likizo unakuwa na pakufikia. Huduma nyingine iliyoanzishwa ni Fahari Huduma ambayo ni Argent Banking.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei.
Akiwa Benki ya CRDB ameingoza kutoka Benki iliyokuwa ikijiendesha kwa hasara hadi kuwa Benki inayoongoza nchini. Dkt. Kimei ni mTanzania wa kwanza kukamata tuzo la zaidi ya miaka kumi iliyopita kutoka kwa African Banker Awards chini ya African Development Bank Group, mTanzania pekee kwenye kinyang`anyiro ambacho kimekuwa kikitawaliwa na mabenki kutoka nchini Nigeria na Afrika ya Kusini.
Nifahari kubwa kwa waTanzania wa DMV kutembelewa na jopo zima la CRDB kwakua kila mmoja anahitajika hazina ya huduma njeema za kuwekeza nyumbani, iwe kwa mikopo ama kwa kipato ambacho amekipigania kwa miaka mingi, ili apate nguvu za kuwekeza nyumbani, kwa sasa imepatikana njia ya mkato kupitia benk yetu ya kizalendo ambayo ina manufaa makubwa kwa wana Diaspora waTanzania wanaoishi nchi mbali mbali kupitia Benki ya CRDB, sasa uwamuzi ni wako Mahojiano na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei na Jamii ProductionKUWENI NA SUBRA.. yatawajia PUNDE...ila ushauri WETU ni Kumsikiza vyema ndio kujua na kufaidika na mpango mzima wa Huduma ya Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kulia) alipofanyiwa mahojiano na Mwanachangamoto yetu kutoka Jamii Production Mubelwa Bandio kuhusu oboreshaji wa huduma ya Tanzanite. Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa. akiwa makini kusikiliza Mahojiano ya Jamii Production Siku ya Jumatano Oct 9, ofisi ya Ubalozi Jijini Washington DC.
Mkurugenzi wa Hazina CRDB Bwna Alex Ngusaru akisikiliza Mahojiano ya Jamii Production na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei, Siku ya Jumatano Oct 9, ofisi ya Ubalozi Jijini Washington DC.
Mortgage Finance Speccialist wa Bank Of Tanzania (BOT) Baraka Munisi akisikiliza Mahojiano ya Jamii Production Siku ya Jumatano Oct 9, ofisi ya Ubalozi Jijini Washington DC.
Ofisa wa ubalizi wa Tanzania Nchini Marekani Bwna Suleiman Saleh akisikiliza Mahojiano ya Jamii Production na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei, Siku ya Jumatano Oct 9, ofisi ya Ubalozi Jijini Washington DC.
Kwa Mahojiano ya Jamii Production na Mkurugenzi wa Benki ya CRuDB Dkt. Charles Kimei yatawajia hivi punde.
No comments:
Post a Comment