TUMEHAMA / WE HAVE MOVED

TAFADHALI TEMBELEA TOVUTI YETU MPYA WWW.JAMIIPRODUCTION.COM (bofya hapa)

PLEASE VISIT OUR NEW WEBSITE WWW.JAMIIPRODUCTION.COM (click here)

TUMEHAMA. TAFADHALI TEMBELEA TOVUTI YETU MPYA WWW.JAMIIPRODUCTION.COM..........WE HAVE MOVED. PLEASE VISIT OUR NEW WEBSITE WWW.JAMIIPRODUCTION.COM

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA. "Tiba" ya virusi vya UKIMWI kwa mtoto wa pili

Photo Credits: Fox 44
Mwezi wa tatu mwaka jana, madaktari nchini Marekani walitangaza kuwa mtoto mmoja kutoka jimbo la Missisipi nchini humo aliyezaliwa akiwa na virusi vya UKIMWI alitibiwa na kuonekana kutokuwa navyo tena.
Tangazo hilo lilizua mashaka makubwa kuwa yawezekana mtoto huyo hakuwa ameathirika na virusi hivyo licha ya kuwa Mama yake alikuwa mwathirika wa virusi.
Lakini madaktari waliendelea kusisitiza kuwa matibabu maalum waliyompa punde baada ya kuzaliwa yalimtibu.
Wiki hii, katika mkutano unaohusu masuala ya VIRUSI huko Boston, madaktari wametangaza kuwa mtoto wa pili aliyepata aina hiyo ya matibabu punde baada ya kuzaliwa amepimwa na kuonekana kutokuwa tena na virusi hivyo.

Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Machi 8, 2014

No comments:

Post a Comment